AFISA wa Shamba la Miti Wino Saimon Tonoro akimwakilisha Meneja wa Shamba hilo Grory Fotnatus katika Sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Halamshauri ya Madaba ametoa elimu ya upandaji miti na faida zake.
Tonoro amesema TFS Wino wanasimamia upandaji Miti na shamaba hilo linajumla ya Hekta 39 na wameligawa katika safu tatu ikiwa safu ya Wino zipo hekta takribani 2,000,safu ya Ifinga hekta 20,000 na Mkongotema.
Amesema shughuli kubwa ambayo TFS wanaifanya ni upandaji miti na utunzaji wa Mazingira pamoja na ufugaji wa nyuki.
Tonoro amesema Serikali imewekeza kwa nguvu kubwa zoezi la upandaji miti na unafaida nyingi ikiwemo utunzaji wa Mazingira,utunzaji wa vyanzo vya Maji,upatikanaji wa nishati ya umeme.
Amesema Kubwa zaidi ambayo Serikali inaliangalia kwa ukubwa ni upatikanaji wa kipato upandaji Miti unafaida kubwa chanzo cha Mapato Serikalini na Watu binafsi.
“Wengi wetu ni mashaidi naamini mlishawahi kufika Mji wa Mafinga shamba lile tulianza kama ilivyo wino sasaivi watu wameanza kuvuna na fursa zinafunguka watu watapata ajira”.
Hata hivyo amesema kiuhalisia watu walikuwa wakipanda miti hivyo ukipata maelekezo sahihi baada ya miaka michache utapata faida na kabla hujapanda lazima ujue unapanda kwa lengo gani.
Amesema ukitaka kupanda Miti lazima uandae eneo vizuri kwa kufyeka pamoja na kuzingatia taratibu za uchomaji moto ,na kusubili msimu wa mvua kuanza.
“Hekta Moja inabidi upande miti 1111 kupanda miti mingi ndani ya eneo moja siyo kupata faida miti haita nenepa kwenye hekari 544 miti hadi mti mita 3”.
Amesema ukisha panda lazima ihudumiwe inadidi ipaliliwe na kuzungushia barabara ya moto ili moto usiingie ndani ya shamba mita 10 pamoja na kufyekea.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Septemba 28,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa