KUFUATIA Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Afisa Ustawi wa Jamii Shani Kambuga na Afisa Lishe John Mapunda Halmashauri ya Madaba wametoa Elimu kwa Jamii.
Afisa ustawi amesema kuna taasisi tatu ikiwemo ngazi ya familia inayohakikisha watoto wanalelewa ambayo inaishi na watoto kwa Mda mwingi hivyo Familia ikilegalega watoto hawawezi kupata haki yao ya msingi.
Kambuga amesema Taasisi ya Pili ni jamii ambayo kimsingi inatakiwa kuhakikisha mtoto analindwa na kuwalea pamoja na kuwatunza, jamii ikipuuzia husababisha ukatili wa watoto ikiwa Taasisi ya tatu ni Serikali inawajibika kuwatunza na kuwalea watoto hao.
“Wananchi tunawaombeni sana Familia,Jamii pamoja na Serikali tuungane ili tuweze kuwalea watoto kwa pamoja kwa malezi bora hao ndio Taifa letu la Kesho Mh. Rais Samia amekuwa akisisitiza sana kupinga ukatili dhidhi ya watoto”.
Kwa upande wake Afisa Lishe John Mapunda amesema kupitia siku ya mtoto wa Afrika idara ya Afya wamekuwa na jukumu la kusimamia haki ya msingi ya mtoto kwa kupatiwa Matibabu na Lishe.
Mapunda amesema kwa kutambua hivyo wanasimamia mpango wa Serikali wa 2021 mpaka 2026 jukumu kubwa kuzuia tatizo la upungufu wa uzito hasa kwa watoto na tatizo la ukosefu wa Madini na vitamini.
“leo katika banda letu tunatoa huduma ya matone ya vitamini A kwa watoto chini ya miaka 5 na tathimini ya hali ya Lishe kwa watoto kuanzia miaka 5 hadi 18”.
Amesma wanafanya hivyo kwa lengo la kujua hali zao kwa sababu wapo katika misingi ya Elimu wakiwa na lishe duni ufaulu wao hautakuwa mzuri na tutasimamia kwa kutoa ushauri na huduma ya chakula Mashuleni.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 16,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa