• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAAFISA Ugani na Maafisa Ushirika wapatiwa pikipiki 286 Ruvuma

Posted on: June 14th, 2022

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge awaonya maafisa ugani  kuepuka matumizi  mabaya ya pikipiki za Serikali.

Hayo amezungumza katika hafla fupi ya ugawaji wa pikipiki 286 kwa maafisa Ugani na Maafisa Ushirika wa Mkoa  huo katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ibuge amesema Mkoa wa Ruvuma unategemea Kilimo zaidi ya asilimia 87 kwa wakazi na shughuli hizo kuchangia pato la Taifa na Mkoa.

Amesema shughuli hizo za Kilimo pamoja na uvuvi takwimu ya Taifa ya mwaka 2019 Mkoa umechangia pato la Taifa  kwa Mwaka kiasi cha zaidi ya shilingi tilioni nne sawa na wastani wa asilimia 3.8 na Mkoa kushika nafasi ya 10.

“ Rais wa Jamhuri ya Muungano  ameona changamoto  za Wataalam wa kilimo na ushirika na kutupatia pikipiki 7000 kwa nchi ya Tanzania  na vifaa vya upimaji wa udongo kwa maafisa ugani Kata na Vijiji”.

Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Ruvuma umekuwa kinara kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kwa miaka mitatu mfululizo,uzalishaji huo umetokana na wakulima maeneo makubwa ingawa  tija ya uzalishaji katika maeneo kuwa mdogo.

“Mkoa wetu wa Ruvuma tumebahatika kupata Mgao wa Pikipiki  286 tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kuona changamoto hii na kuwezesha ununuzi wa pikipiki na vitendea kazi vya kilimo kwa maafisa ugani”.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma Pololeti Mgema amesema asimia 75 ya watanzania wanategemea Kilimo.

Mgema amesema Kilimo ni Biashara kikiwa na tija  hivyo ametoa rai kwa wataalamu kufanya kazi kwa bidii ikiwa kuacha kukaa katika ofisi na kwenda katika maeneo ya wananchi kuwapatia elimu ili waweze kuzalisha kwa tija.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde na Jackson Mbano

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Juni 14,2022

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa