MAADHIMISHO ya Siku ya Kimataifa ya uelewa kuhusu Ualbino Kitaifa yamefanyika Mkoani Ruvuma.
Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana ,Ajira na watu wenye ulemavu Joyce Ndalichako ,ambapo amewakilishwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile.
Ndile katika hotuba yake amesema Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa ambayo haijapata tukio la udhalilishaji kwa watu wenye ualbino kama mikoa ya Kanda ya Ziwa.
“Hii kama mlivyoona katika Mkoa wa Ruvuma yangeweza kufanyika lakini kwaajili ya uongozi thabiti na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuwa waungwana na Mkoa umeendelea kuwa na amani na utulivu”.
Amesema Serikali imewapa kipaumbele wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na maswala ya Elimu na uwezeshwaji wa kiuchumi,Afya, Ajira , mafunzo ya ufundi stadi pamoja na nyenzo za kujimudu.
“Serikali ya awamu ya sita imeendelea na utekelezaji wa huduma ya watu wenye ulemavu Nchini imezingatia Sera,sheria,mikataba ya kikanda na Kimataifa”.
Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi Ralph Meela amesema mara baada ya kuwepo kwa matukio mbalimbali kuanzia mwaka 2006 hadi 2017 matukioa ambayo yalitambuliwa na Jeshi la Polisi Nchini yalikuwa 73 ambayo yalitambuliwa na kushirikisha imani za kishirikina.
Hata hivyo Meela ameipongeza Serikali kwa Juhudi zinazosimamiwa na Rais akiwa ni amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Nchini kwa kuhakikisha watu wenye ualbino wanakuwa salama.
“Mimi niseme tu kwa wenzetu wenye ualbino hali ya usala ni shwari tunawapa moyo na matumaini ulinzi umeimarishwa pande zote juhudi zilizofanywa na Serikalikwa kutoa Elimu”.
Hivyo amesema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi ni sawa kama wanadamu wengine ikiwa katika matukio 73 matukio 54 yalitokea kanda ya Ziwa kwaajili ya uchimbaji wa Madini na uvuvi wa Samaki.
Amesema Jeshi la Polisi wamechukua hatua ya kukamata waganga wapiga lamri chonganishi kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 walifanya oparesheni ya kukamata hao na matunguli yao wengine wamefungwa na wengine mpaka sasahivi wanatumikia vifungo vyao.
“Nitoe wito kwa watu ambao wanaona watu wenye ualbino viungo vyao vinaweza kuongeza lolote katika maswala ya kiuchumi siyo kweli, wenzetu wenye ualbino waendelee kufanya shughuli zao tuna walinda na wahalifu waache mara moja tabia ya kutumia viungo vyao”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa