• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MAADHIMISHO ya Sherehe ya miaka 60 ya Uhuru yafana Ruvuma

Posted on: December 9th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameongoza Sherehe za maadhimisho ya Miaka sitini ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Sherehe za Maadhimisho hayo imefanyika katika  Viwanja vya Shule ya Muhuwesi Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Ibuge amesema  Miaka 60 iliyopita Tanzania Bara ilikata minyororo  ya ukoloni Mwaka 1961  Mwasisi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwaongoza wananchi wa Tanganyika katika kuupokea uhuru.

’’Siku hiyo aibu ya takribani Miaka 77 ya kutawaliwa na wageni kutoka Ulaya ilifikia Ukomo tumetawaliwa na Waingereza Miaka 43 (1918-1961) na kabla yao  miaka 34  (1884-1918) ya ukoloni wa Ujerumani’’.

Hata hivyo ibuge ameelezea mafanikio tangu kupata Uhuru Tanzania hadi kufikia sasa ikiwemo sekta ya Elimu hali ya Kielimu ilikuwa duni sana hivyo watu wengi walikuwa wanakabiliwa na ujinga.

Amesema Mwalimu Nyerere alitangaza ujinga kuwa moja ya maadui watatu ya nchi yetu pamoja na umaskini na maradhi,ilisababishwa na ufinyu wa kupata Elimu hasa kwa Waafrika ikisababishwa na Serikali ya Kikoloni.

’’Wakati tunapata Uhuru Mkoa ulikuwa na Shule za msingi 46 leo hii Mkoa una shule za msingi 818,shule za Sekondari zilikuwa 3 mpaka kufikia sasa Mkoa unashule za Sekondari 214, takwimu zinaonyesha mafanikio na kutufanya tutembee kifua mbele’’.

Akizungumzia upande wa Sekta ya Afya amesema mwaka 1961 Mkoa ulikuwa na Zahanati 8 na Hospitali 4 lakini mpaka kufikia sasa Mkoa wa Ruvuma una vituo 348 vinavyotoa huduma za Afya ikiwemo Zahanati 301 Vituo vya afya 34 na Hospitali 13.

Ibuge amezungumzia swala zima la Umeme  kabla ya Uhuru  mwaka 1961 hali ya upatikanaji wa Nishati ya Umeme ilikuwa Duni kwani isipokuwa baadhi ya maeneo machache,kwa sasa Mkoa umeunganishwa Umeme wa gridi ya Taifa katika Wilaya zote ikiwemo vijiji 319  vimepata na vijiji 235 vipo kwenye mpango.

Amesema sekta ya Miundombinu kabla ya  Uhuru ulipopatikana Mkoa wa Ruvuma haukuwa na Mtandao wa Barabara za kiwango cha lami kwa sasa Barabara  zina kiwango cha lami kilomita 700 za Barabara  za kiwango cha lami ambapo Wilaya zote 5 zimeunganishwa katika kiwango cha lami.

  Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Desemba 9,2021.                   

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa