KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2023 Abdalla Shaib Kaim amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kusimamia miradi ya Maendeleo kwa weledi.
Kaimu mara baada ya kufungua madarasa mawili yaliyojengwa kwa shilingi milioni 40 fedha kutoa Serikali kuu amesema ameridhishwa na miradi hiyo.
Kiongozi huyo ameendelea kuwapongeza viongozi hao kwa kuunga mkono kauli mbiu ya utunzaji wa mazingira iliyopo katika swala nzima la uhifadhi na utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti,utunzaji wa bustani na kupanda miche ya miti katika maeneo ya Shule hiyo.
“Tumekagua nyaraka tumejiridhisha zinakidhi viwango vyote kwahiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru nakili fedha imetumika vizuri na tumeridhika na mradi”.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Madaba Innocent Kalesa amesema Octoba 01,2022 walipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 40 kwaajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
Kalesa amesema ujenzi ulianza rasmi Octoba 18,2022 na kukamilika Desemba 4,2022 kwa kutumia force account ambapo shule ilinunua vifaa na kuajili fundi wa ujenzi na kusimamiwa na kamati tatu.
Mkuu wa Shule amezieleza faida za mradi huo ikiwa ni pamoja na kupatiwa vyumba bora vya madarasa na kuwezesha uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 117 ,2023.
Kupatiwa kwa samani bora kwa wanafunzi wakati wa kujifunza na kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Aprili 19,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa