Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim ameweka jiwe la Msingi katika Kikundi cha vijana cha kufyatua tofali cha Madaba kwetu kilichopewa Mkopo wa asilimia 10 unaotokana na Mapato ya ndani.
Kiongozi huyo mara baada ya kuweka jiwe hilo la Msingi ameipongeza Halmashauri kwa kuunga Mkono Kauli mbiu ya utunzaji wa Mazingira pamoja na kuwawezesha vijana na makundi ya watu wenye mahitaji maalumu na kutekeleza maagizo kutoka Serikali kuu.
“Tumekagua mradi na nyaraka tumeona vigezo na ubora vimezingatiwa na mradi unauhalisia ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira mmefanya vizuri tuwapongeze vijana hawa”.
Kaim ametoa rai kwa vijana kutumia fursa pamoja na kubuni miradi ya maendeleo mbalimbali ikiwa kujiajili na kuacha kujishughulisha na kazi ya wizi,ujambazi na madawa ya kulevya.
“Serikali inadhamira ya dhati fedha ipo nyingi inatolewa kwa kukopesha sambamba na fedha inayotolewa na Halmashauri upo mfuko wa uwezeshaji kupitia mfuko wa Waziri Mkuu tunakopesha mtu mmoja mmoja,kikundi mpaka Kampuni hadi kufikia milioni 50 vijana wenzangu walichokifanya ni fursa na uzalendo mkubwa”.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ametoa rai kwa vijana wa kitanzania kuiga na kutumia fedha hizo kwa kujikwamua na kujipatia ajira.
Hata hivyo ameendelea kutoa rai kwa vijana wa kikundi hicho kurejesha marejesho kwa wakati ili na wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo,pia amewaomba viongozi wa Halmashauri kuwapa kipaumbele cha tenda zinazojitokeza katika Halmashauri hiyo.
Katibu wa kikundi hicho Tumaini Wendalage akisoma taarifa kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2023 amesema Halmashauri wamewakopesha kiasi cha shilingi milioni 44 ambazo zimewawezesha kujenga ofisi pamoja na ununuzi wa Mashine ya umeme yenye uwezo wa kufyatulia matofali 1000 kwa siku.
Hata hivyo wendalage ameeleza kikundi hicho kina wanakikundi 8 wakimwemo vijana wa kike 5 na vijana wa kiume 3 ,pia amesema kupitia kikundi hicho kitasaidia kutoa ajira kwa vijana wengine katika Halmashauri ya Madaba
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Halmshauri ya Wilaya ya Madaba
Aprili 19,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa