• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

Kiongozi wa Mbioa za Mwenge aipongeza Halmashauri ya Madaba kwa ujenzi wa Madarasa yenye viwango

Posted on: September 6th, 2021

MRADI wa Madarasa mawili ya shule ya Msingi Mtyangimbole umezinduliwa na kiongozi wa Mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru Lt Josephine Mwambashi na ametembelea mradi wa lishe pamoja na kukagua banda la Malaria.

Ujenzi wa Madarasa hayo umegharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 40 kutoka Serikali kuu na nguvu kazi za Wananchi shilingi milioni 5.5, na kubaki shilingi zaidi ya milioni 4 na kutumika kukarabati madarasa mengine.

Mara baada ya kuzinduliwa kwa Madarasa hayo Kiongozi huyo amesema umuhimu wa madarasa hayo yataongeza ari  ya wanafunzi kupata hamasa ya kujisomea kwa usahihi na amewaagiza wanafunzi kutumia vizuri na wengine wajao watumie.

Mwambashi ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kusimamia mradi huo kwa viwango vinavyotakiwa na kuhakikisha kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 4 kinabaki na kutumia  kukarabati madarasa mengine ya shule hiyo.

“Gharama za mradi huo tulipokea fedha kutoka Serikali kuu milioni 40 na nguvu ya wananchi ni milioni 5.5, mradi huo umejengwa kwa kutumia force account”.alisema Mkurugenzi wa Halmashauri.

Wakati huo huo katika kuboresha afya ya wananchi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed ameuongea  mradi wa lishe ikiwemo siku ya afya ya Lishe ya kijiji cha Likalangilo,ambayo ni mpango  jumuishi ya kuboresha upatikanaji wa Afya kwa jamii na kuwajengea uwezo wa kutambua jinsi ya kuzuia utapiamlo.

 Amesema Wilaya ya Songea inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu lishe bora na umuhimu wa Lishe bora katika familia na jamii kwa ujumla kwa kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo klini ya kila mwezi kwa wazazi na walezi wa watoto chini ya miaka mitano,siku za afya za Lishe zinazofanyika kila robo ya mwaka.

Hata hivyo ameelezea wananchi wa Halmashauri ya Mdaba  wanavyoelewa umuhimu wa Lishe na wanaendelea kuwafahamisha juu ya umuhimu wa lishe bora na athali zitokanazo na lishe duni na madhara ya utapia mlo.

Vile vile Mkurugenzi  kwa upande wa Malaria amesema Ugonjwa wa malaria ni miongoni mwa Magonjwa 10 yanayoongoza kuhatarisha  maisha ya jamii katika Wilaya ya Songea.

“Hali ya maambukizi imepungua kwa wastani wa kutoka asilimia 11.5 mwaka 2019  na kufikia asilimia 8.1 mwaka 2021,hii ni kutokana na hatua mbalimbali ambazo zilikuwa zikichukuliwa  na idara ya afya”.

Ameelezea utekelezaji wa kuhakikisha Ugonjwa huo unadhibitiwa kwa matibabu kwa kutumia kanuni na miongozo  ya Wizara ya Afya kwa walewanaobainika wameambukizwa Uganjwa kwa wajawazito wanaoanza kliniki na watoto chini ya miaka mitano.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa habari Halmashauri ya Mdaba

Septemba 6,2021.

 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa