HALMSHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya kikao cha Baraza cha robo ya kwanza mwaka 2023/2024 cha kujadili vikao vya kamati tano ikiwemo kamati ya Maadili,kamati ya kudhibiti UKIMWI,kamati ya huduma za jamii kamati ya uchumi na mazingira na kamati ya fedha.
Katika Baraza hilo ameapishwa Diwani mpya wa kata ya Mtyangimbole Twahib Ngonyani kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika Septemba 19,2023 baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo kufariki.
Amina Tindwa ambaye ni Afisa tawala akimwakilisha Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma Peniel Mbura akitoa salamu katika Baraza hilo amempongeza Diwani wa Kata ya Mtiyangimbole kwa kula kiapo tangu alipochaguliwa na kupata ushindi wa asilimia 97.
“Kiapo hiki kinamaana kubwa sana mimi nakusihi ukazingatie yale uliyoelekezwa lakini unajukumu kubwa la kuwadhihirishia Wananchi wako waliokuchagua kuwa unaweza kushirikiana nao”.
Tindwa amewapongeza Wataalam wa Halmashauri hiyo kwa ushirikiano wanaotoa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo nakuhakikisha miradi ya Maendeleo inakamilika kwa wakati.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba Novemba 11,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa