HALMASHAURI ya Wilaya ya madaba inawakaribisha wananchi wote kujifunza ufugaji wa Kuku kuchi (Asili).
Ujifunzaji huo unapatikana katika banda lililopo viwanja vya maonyesho ya Nane nane vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Mfugaji wa Kuku hao kuchi kutoka Jiji cha Ngadinda kata ya Ngumbiro Halmashauri ya Madaba Kuluas Mayombe amesema kuwa kuku hao wanafaida sana kwasababu Tanzania hawapatikani wengi.
Amesema kifaranga kinauzwa kwa shilingi elfu 70,000/= Kuku mkubwa anauzwa kwa kiasi cha shilingi laki 6 hadi laki 7 kwasababau wanakilo nyingi na wanamanyoya machache kuliko kuku wa kawaida.
Hata hivyo amesema yai moja la kuku huyo linauzwa kwa shilingi elfu 10,000/= na kuku hao ni wakali tofauti na kuku wa kawaida ambao wanatumia kwaajili ya kuchezesha kamili ya kupigana.
“Tunawakaribisha wananchi wote kuja kujifunza katika banda letu la Halmashauri ya Madaba viwanja vya Nane nane”.
Kutoa kitengo cha Mawasiliano Hahalmashauri ya Madaba
Agosti 5,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa