SERIKAI ya awami ya Sita inayoongozwa na Rais Samia imetoa shilingi Milioni 50 kwaajili ya umaliziaji wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Halmashauri ya Madaba.
Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Oddo Mwisho wametembelea na kukagua mradi huo ulianzishwa kwa nguvu za wananchi kwa ufyatuzi wa tofari Mwaka 2022 Julai kwa hatua ya Msingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema walitoa Milioni 31 ya Mapato ya ndani kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya Viwandani pamoja na malipo ya fundi na ukamilishaji wa boma.
Amesema Wawekezaji waliowekeza katika kijiji hicho akiwemo Mufindi woodpoles Planting Timber Ltd walitoa Milioni 10 pamoja na mifuko 200 ya saluji na Shamba la Miti Wino TFS walitoa Mifuko 150 ya Saluji ambayo imetumika kupiga lipu jengo hilo.
“Tumepokea Shilingi Milioni 23,676,000 kutoka kwa Mwekezaji Mufindi Woodpoles planting timber Ltd kwaajili ya ununuzi wa Mbao na bati za kuezekea Jengo ”.
Mwisho amewapongeza wawekezaji waliowekeza katika Kijiji cha Ifinga,Serikari ya awamu ya sita na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kujali miradi inayoanzishwa kupitia nguvu za wananchi na kuikamilisha.
Imeandaliwa na Aneth ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halamshauri ya Madaba
Oktoba 9,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa