KAMATI ya kudumu ya Bunge Utawala Katiba na Sheria imetembelea eneo la uwekezaji wa kilimo cha Mbegu shamba la Silver land Ndolela lenye Hekta 5000 Jimbo la Madaba.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati, Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama amesema Wabunge wamepata fursa ya kutembelea eneo la uwekezaji wa kilimo cha mbegu Jimbo la Madaba.
“Tumepata fursa ya kutembelea sekta ya viwanda lakini Waheshimiwa Wabunge hawakupata fursa ya kutembelea kwenye sekta ya kilimo,huwezi kuchukua changamoto ya viwanda kuleta kwenye kilimo itakuwa vizuri Kamati inapoenda kuandaa bajeti ijue changamoto ya sekta hii”.
Mhagama amesema ziara yao katika eneo hilo imeleta fursa ya kujifunza ili waweze kushauri serikali kuhusu sekta hii.
“Tunajua vikwazo mbalimbali Wabunge wengi tunatoka kwenye familia ambazo wanalima lakini pengine hatujapata fursa ya kujifunza uwekezaji katika sekta ya kilimo kwa kiwango kikubwa”.
Hata hivyo Mhagama amesema uwekezaji huo utaimalika zaidi kama barabara ya kutoka Madaba na kuungana na Wilaya ya Ludewa itatengenezwa kwa kiwango cha Lami ikiwa kuna fursa ya uchimbaji wa chuma na wananchi wanaofanya kazi katika maeneo haya wanachukuliwa katika Kijiji cha Madaba na Mavanga ambao ni Halmashauri ya Ludewa Mkoa wa Njombe.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Machi 14,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa