SERIKALI ya awamu ya sita imeleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 95 kwaajili ya ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Sekondari Jeseph Mhaga Halmashauri ya Madaba.
Kamati ya Fedha ya Halmashauri hiyo wametembelea na kukagua mradi huo uliofikia asilimia 82.6 ya ukamilishaji wa mradi huo.
Mkuu wa shule hiyo Vermund Kapinga akisoma taarifa amesema Juni 19,2023 walipokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 95 kwaajili ya ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu kupitia mradi wa SEQUIP.
Kapinga amesema mradi huo umeanza kutekelezwa Septemba 11,2023 kwa kujenga msingi na kufikia sasa ujenzi umefikia hatua ya kuweka malu malu na kuskimu.
“Hadi kufikia sasa tumetumia kiasi cha shilingi Milioni 82 na kubakiwa na zaidi ya shilingi Milioni 12 ,na kukamilika ifikapo tarehe 20 mwezi wa 11,2023”.
Hata hivyo Mkuu wa Shule hiyo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa nyumba ya Mwalimu itakayosaidia kupunguza umbali wa makazi ya walimu na uangalizi wa wananfunzi kwa ukaribu zaidi.
Kutoka kitengo cha Mawasilino Halmashauri ya Madaba
Novemba 7,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa