SERIKALI imeleta Fedha kiasi cha shilingi Milioni 128 kwaajili ya Ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Madaba Halmashauri ya Madaba.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Shule Victor Luoga kwa Kamati ya Fedha walipotembelea Mradi huo amesema mradi umefikia asilimia 95 na hadi kufikia sasa fedha zilizotumika Milioni 113,174,765.42.
Luoga amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika Januari 30,2024 na kuanza kutumika ikiwa katika Halmashauri ni kituo pekee cha wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Kamati ya Fedha wameshauri kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuzingatia kila eneo la umaliziaji linakamilika kwa wakati na ubora.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmshauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 23,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa