• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

KAMATI ya CCM yatoa wiki moja mradi wa maji Madaba kutoa majia

Posted on: April 20th, 2021

KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma imetoa wiki moja kwa TANESCO kuhakikisha wanapeleka umeme kwenye mradi wa maji Madaba wilayani Songea ili wananchi waanze kunufaika na maji safi na salama.

Akizungumza baada ya kamati hiyo kukagua mradi wa maji Madaba ambao serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kutekeleza mradi huo,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Oddo Mwisho amesema mradi huo umechukua muda mrefu ambapo hivi sasa serikali imedhamiria wananchi wa Madaba kupata maji na salama.

“Nampongeza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma ambaye ndani ya muda mfupi amesimamia miradi mingi ya maji iliyosababisha Mkoa wa Ruvuma kupata tuzo ya umahiri wa kusimamia miradi ya maji’’,alisema Mwisho.

Kwa niaba ya Kamati, Mwisho amewaagiza TANESCO Ruvuma kuhakikisha wanashughulikia umeme ili kuanzia wiki ijayo wananchi wa Madaba waanze kupata maji na kwamba Kamati ya Siasa haihitaji ubabaishaji katika kushughulikia suala ya kero ya maji kwa wananchi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameutaja mradi wa maji Madaba kuwa ni wa zamani na kwamba wananchi wamepata shida kwa muda mrefu.

Hata hivyo amesema RUWASA Mkoa wa Ruvuma wamefanya kazi kubwa  ya kutekeleza mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika kwa asilimia 100.

Hata hivyo Mndeme amesema TANESCO wamechangia kuchelewesha mradi huo ambapo ametoa siku tano kuhakikisha wanamaliza kazi ya kupeleka umeme kwenye mradi huo na pasiwepo na kisingizio chochote.

“Wananchi wa Madaba hivi sasa wanahitaji maji,mimi nitapita hapa Alhamis,nikifika TANESCO hamjafanyakazi nitawaweka ndani wote,nataka tumalize huu mradi,TANESCO mkinizingua,tutazinguana,kila mtu avae sura ya kazi’’,alisisitiza Mndeme.

Awali Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mathias Charles  amesema mradi huo hadi sasa umefikia zaidi ya asilimia 90 ambapo amezitaja kazi zilizokamilika kwa asilimia 100 ni ujenzi wa tanki la juu la kuhifadhia maji kwenye kijiji cha Lituta lenye ujazo wa lita 50,000.

Kazi nyingine zilizokamilika ni ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Kipingo lenye ujazo wa lita 100,000 na kwamba ujenzi wa vituo 21 kati ya 40 vya kuchotea maji vimekamilika na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi umekamilika  kwa asilimia 98.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Olaph Pilly kwa niaba ya wananchi wa Madaba ameipongeza serikali kwa kutekeleza mradi huo wa maji ambao utaifanya kero ya maji Madaba kubakia historia.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Aprili 20,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa