NAIBU Katibu Mkuu wa (OR Tamisemi ) Ramadhan Kailima amefanya kikao kazi na viongozi wa Sekretalieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Wakuu wa Idara katika swala la kuzungumzia hali ya ufutaji wa hoja za ukaguzi.
Kikao kazi hicho kimefanyika katika ukumbi wa Manispa ya Songea Mkoani Ruvuma na kujumuisha Viongozi wa Halmashauri zote.
Akizungumza Katika kikao kazi hicho ametaja vipaumbele vya ufutaji wa hoja za ukaguzi na maagizo yaliyotolewa na kamati ya Kudumu ya Bunge la Hesabu za Serikali za Mitaa.
Kailima amesema hoja za Serikali zikifutwa miradi mbalimbali ya Serikali itaendelea vizuri ikiwemo Vyumba vya Madarasa,Vituo vya Afya na mingine.
“Sitakuwa na Msamaha na Mtendaji yoyote ambaye atakuwa anazalisha hoja kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na wala usitegemee kuhamishwa na kupewa nafasi nyingine hapo ulipo”.
Hata hivyo Kailima amesema watumishi wanaodai madai yao ya likizo walipwe ili wafanye kazi kwa bidii.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Madaba
Novemba 14,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa