JENGO la Ofisi ya Uthibiti bora wa shule za Halmashauri ya Madaba lililogharimu zaidi ya shilingi Milioni miamoja linatarajia kukamilika Desemba 2020.
Akitoa taarifa hiyo Mthibiti Mkuu wa Elimu bora wa Shule Halmashauri ya Madaba Godlove Makongwa ofisini kwake amesema wamepokea fedha kutoka serikali kuu kwaajili ya ujenzi wa Ofisi na ujenzi umeanza septemba 22,2020.
“Tuna mshukuru sana Mh.Rais kuhakikisha Wilaya zinakuwa na Ofisi za Uthibiti Bora wa Shule nchi nzima na sisi Halmashauri ya Madaba tumekuwa miongoni mwao”.
Makongwa amesema katika Halmashauri ya Madaba wapo watumishi sita ambao wameanza kufanyakazi Mei 2020 na baada ya kulipoti na kuanza kazi wakatumiwa fedha kwaajili ya ujenzi wa ofisi hiyo.
“Selikari ya awamu ya tano imejitaidi kuweka mazingira mazuri kwa watumishi ikiwa pamoja na Uthibiti bora wa Elimu na kuwepo kwetu hapa tukishirikiana na Halmashauri tutafanya kazi vizuri,tutahakikisha suala la Elimu lina songa mbele”.
Hata hivyo Makongwa amesema malengo ya kujenga ofisi ya Uthibiti bora wa Shule ni kuwa na mazingira Mazuri ya Kazi na hatimaye kupata nafasi ya kufuatilia shule za Halmashauri ya Madaba katika Nyanja mbalimbali na utekelezaji wa sera ya Elimu.
Kwa Mkoa wa Ruvuma Mwaka 2019 Wilaya tano zilipatiwa fedha na kujenga ofisi ya uthibiti bora wa shule na mwaka huu 2020 Wilaya mbili zimepewa fedha kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi hizo za Uthibiti bora wa shule ikiwemo Wilaya ya Madaba na Wilaya ya Mbinga.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari wa Halmashauri ya Madaba
Desemba 21,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa