UJENZI wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba ambalo limegharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili limekamilika kwa asilimia 99.
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake Mhandisi wa Halmashauri hiyo Ludger Nchimbi amesema ujenzi wa jengo hilo, ulianza rasmi mwaka 2017 na kwamba mradi umejengwa kwa awamu tatu.
Amesema katika awamu ya kwanza mkataba ulikuwa unatekelezwa na Mkandarasi Wakala wa Majengo Tanzania TBA,ambao uligharimu zaidi ya shilingi milioni 493,awamu ya pili ni mkataba wa zaidi ya bilioni mbili na awamu ya tatu ujenzi umefanyika kwa force akaunti kwa ajili ya umaliziaji wa mradi huo.
“Tulipokea fedha kutoka serikali kuu Bilioni tatu ambazo zimetumika kutoka mapato ya ndani, fedha iliyotumika mpaka kukamilika Jengo shilingi zaidi ya shilingi bilioni mbili’’,alisema.
Hata hivyo Mhandisi amesema Mkandarasi TBA alisimamishwa kuendelea na kazi ya ujenzi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme Juni 6 mwaka huu,baada ya Mkandarasi huyo kupata changamoto ya kufungiwa akaunti zake zote na kushindwa kuendelea na kazi,hali iliyosababisha Halmashauri kutumia force akaunti kukamilisha mradi huo.
Amesema mradi wa jengo hilo kwa sasa limekamilika na tayari limeanza kutumika kuanzia Oktoba 21, 2020.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauli ya Madaba
Oktoba 27,2020
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa