• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

IDARA ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma yakusanya maduhuli ya Serikali kwa asilimia 108

Posted on: March 1st, 2021

KAIMU Kamishina wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma Ildeforce Ndemela amesema Idara ya ardhi mkoani Ruvuma imekusanya maduhuli ya serikali kwa asilimia 108.

Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelina Mabula,Kaimu Kamishina wa ardhi amesema kiasi hicho cha fedha kimekusanywa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.

Ndelema amesema serikali iliupangia Mkoa wa Ruvuma kukusanya maduhuli ya serikali ya shilingi 990,000 hadi kufikia Juni 30,2020 na kwamba Idara ilifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1,076,957,355.22 sawa na asilimia 108.

“Katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 Idara ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma imepangiwa lengo la kukusanya kiasi cha bilioni 4.6, hadi kufikia Februari Mkoa umekusanya shilingi milioni 740 sawa na asilimia 16,mikakati ya kuongeza makusanyo ya kodi ikiwemo ikiwemo kuandaa na kusambaza ankra za umiliki na Hati za madai ya kodi’’,alisema Ndemela.

Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma katika kipindi mwaka 2020/2021 umepangiwa lengo la kupima viwanja 16,550 na mashamba 104 ambapo hadi kufikia Februari 22,2021,viwanja 4,873 na mashamba matano yamepimwa katika maeneo ya mijini na vijiji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Amesema Idara hiyo imepokea jumla ya michoro ya mipango miji 41  yenye jumla  ya viwanja 18,581 vya matumizi mbalimbali na kwamba zoezi la kurasimisha makazi holela linaendelea katika Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelina Mabula akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo amesema ukusanya maduhuri ya serikali kitaifa katika Wizara yake  imefikia asilimia 30 na Mkoa wa Ruvuma umefikia asilimia 16.

Kutokana na hali hiyo Naibu Waziri Mabula ameziagiza Halmashauri zote nchini kuongeza juhudi za ukusanyaji maduhuli ya serikali ili kufikia malengo waliojiwekea ikiwemo kukusanya madeni kwa kuzingatia sheria.

“Sheria ipo wazi,kifungu cha 50 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya ardhi namba nne kinampa siku 14 tu mdaiwa anapokuwa amepewa Ilani,ndani ya siku 14 asipoweza kulipa,tunampeleka kwenye Baraza, kinachofuata ni yeye kulipa deni’’,alisisitiza.

Amesema ikishatolewa oda ya kutakiwa kulipa anatakiwa kulipa au kukamata mali zake na kuuzwa ili fedha ipatikane ambapo amewataka watendaji wa Ardhi waache kugeuza ukusanyaji maduhuli kuwa kufanyika kisiasa.

Dkt.Mabula amewaagiza maafisa ardhi kuongeza kasi ya kupima viwanja na mashamba na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa maafisa ardhi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo upangaji, upimaji, umilikishaji.uthamini,usajili wa hati,utatuzi wa migogoro ya ardhi na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Machi,Mosi,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa