• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

HEKTA 39,000 za Miti zapandwa Madaba

Posted on: November 12th, 2021

KAMATI ya Siasa Mkoa wa Ruvuma imetembelea Shamba la Miti Wino katika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea lenye hekta 39,000.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho Mara baada ya kukagua Shamba hilo amebaini changamoto ya barabara kutopitika kwa urahisi wakati wa Mvua na amewaomba TARURA kuangalia uwezekano wa uboreshaji wa  Barabara hiyo.

Mwisho amebaini pia changamoto ya uchomaji wa Moto katika maeneo ya Shamba hilo na ametoa rai kwa wananchi kutoa  taarifa pale wanapotaka kuchoma mashamba yao ili TFS wawape mbinu ili Moto usisambae katika Mashamba hayo.

‘’Wananchi Muwe wastaarabu katika kuchoma Misitu Moto kwasababu TFS wanatoa Elimu halafu wananchi mnakuwa wakaidi mnapelekea kuharibu shamba la miti ambalo linategemewa kuingiza uchumi katika nchi yetu’’.

Kwa upande wake Mhifadhi  Mkuu Shamba la Miti Wino Grory Kasmir akisoma taarifa kwa kamati hiyo amesema hifadhi ya Msitu wa Wino iliendelezwa na TFS mwaka 2010 na kuhusishwa eneo dogo la msitu wa asili wenye ukubwa wa hekta 2,000 na mwaka 2014 hadi 2016 walipata maeneo vijiji vya Mkongotema na finga.

Kasmir amesema kuanza upandaji wa Miti hadi kufikia sasa jumla ya hekta 5,004.6 imepandwa miti ya jamii mbalimbali na sehemu kubwa ni miti ya misindano.

Mhifadhi ameeleza malengo makubwa ya kuanzishwa kwa hifadhi ya msitu wa Wino Pamoja na kuhifadhi mali asili zinazotaka kutoweka na vyanzo vya Maji Lupahila,Lutukila,Luhuhu Pamoja na Ziwa Nyasa.

Hata hivyo Kasmiri ameeleza faida ya Shamba hilo ikiwemo Ajira kwa watumishi wa kudumu 15 wamkataba 7 pamoja na vibarua 4,000 na Mazao ya Biashara kama Mbao,Nguzo za Umeme kwa siku za usoni ili kuongeza mapato ya Serikali Pamoja na kuboresha mazingira.

Mhifadhi ameeleza changamoto zinazojitokeza katika Shamba hilo  ikiwemo matukio ya uchomaji wa Moto kwa kiasi kikubwa na kupunguza usimamizi endelevu wa shamba ,uandaaji wa Mashamba msimu wa Kilimo kwa kutumia Moto.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Novemba 12,2012.

 

 

 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa