HALMASHAURI YA Wilaya ya Madaba imeendelea kupata hati safi mfululizo tangu ilipoanzishwa mwaka 2016.
Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza maalum la kujadili utekelezaji wa hoja za mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Mwenyekiti wa Halmshauri Teofanes Mlelwa amesema mwaka wa fedha 2022 unaoishia juni 30 Halmashauri ya Madaba imepata hati safi.
Mlelwa katika Baraza hilo maalumu amewapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo kwa ushirikiano na ametoa rai kuendelea kuwa na ushirikiano katika utendaji kazi unaopelekea kupata Hati safi kila mwaka.
Hata hivyo amewakumbusha Waheshimiwa Madiwani kusimamia Miradi inayoendelea katika Kata zao ili kuhakikisha Mwaka wa Fedha unaoishia Juni 30,2022 iweimekamilika kwa wakati na kuanza miradi mipya inayoletwa na Serikali.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 22,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa