• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

HALMASHAURI zitenge maeneo ya wakulima na wafugaji

Posted on: September 15th, 2022

MKOA wa Ruvuma umeweka mikakati ya kuzuia migogoro ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Afisa Mifugo wa Mkoa wa Ruvuma Nelson  William amesema Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na chama cha wafugaji (CCWT) waone umuhimu wa kufanya Sensa ya Mifugo.

Amesema mikakati hiyo ikiwemo  kutambua wafugaji na mifugo iliyopo katika kila kijiji ili kujua takwimu sahihi  ya mifugo  katika upangaji wa mipango ya  ardhi,miundombinu ya mifugo  na huduma za jamii.

Hata hivyo amesema Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Ruvuma zione uwezekano wa kufanya utaratibu wa kuwatengea wafugaji  eneo la kuchungia  katika vijiji vilivyoainishwa  kwaajili ya ufugaji  na kuwekewa mipaka ya kudumu.

“Kila Halmashauri ione umuhimu wa kuwaelimisha na kuwahamasisha wafugaji  juu ya umuhimu wa utoaji  wa takwimu  sahihi za mifugo”.

Wiliam amesema Wafugaji na wakulima walio katika maeneo yasiyo rasmi mfano hifadhi ya misitu  ya Muhuwesi,Sasawala na Ushoroba wa Kilimasera waondoke kwa hiari waende katika maeneo yatakayoruhusiwa kuchungia.

“Halmashauri zione uwezekano wa kukamilisha mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijijivyenye wafugaji,wahamiaji wakulima wazawa  na watumiaji wengine”.

Amesema Halmashauri za Mkoa zione umuhimu wa kushirikiana na asasi zingine kwa mfano MVIWATA,RUCODIA,PASS,pamoja na wadau wenginewa maendeleo na makundi ya wafugaji ,chama cha wafugaji  katika zoezi la uandaaji wa mipango  ya matumizi bora ya ardhi.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa