Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ni miongoni mwa Halmashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma imeanzishwa na Serikali kwa Tangazo la namba 221.
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassimu Mpenda amesema Halmashauri iligawanyika kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea maeneo ya Utawala wa Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Juni 5,2015.
“Inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa Upande wa Kusini,Wilaya ya Mbinga kwa upande wa Kusini Magharibi,Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe upande wa Magharibi, Wilaya ya Njombe upande wa Kaskazini Magharibi,Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Upande wa Kaskazini na Wilaya ya Namtumbo upande wa Mashariki”.
Halmashauri ya Madaba inakadiliwa kuwa na kilomita za mraba 6,673.97 inasifa ya kuwa na Mvua za kutosha zinanyesha kati ya mm 800 na mm1200 ambazo zinafaa kwa kilimo na Joto la wastani na kubadilika kutokana na nyakati na kufikia wastani wa 20 wakati wa Joto kali kati ya 15 na 17 wakati wa usiku.
Hata hivyo katika Halmashauri hiyo eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 368,704 ambalo sawa na asilimia 55.23 na eneo linalotumika kwa Kilimo mpaka sasa ni hekta 99,580 ambazo sawa na asilimia 27.01.
Amesema Halmashauri ya Madaba inajumla ya vijiji 22,Kata 8 na Tarafa pia Halmashauri inajumla ya Waheshimiwa Madiwani 11 na Mheshimiwa Mbunge 1 kati ya hao 8 wakuchaguliwa na watatu ni wawakilishi viti maalumu.
Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012,Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa mwaka 2019 inakadriliwa kuwa na watu 55,432 kati ya hao Wanaume 27,520 na wanawake 27,912 na kunaongezeko la idadi ya watu la asilimia 1 kwa maeneo ya vijijini kwa kila mwaka.
Halmashauri ya Madaba inamaeneo mazuri ya Kilimo cha Mazao Mbalimbali ya Chakula na Biashara na Maeneo ya Viwanda.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Novemba 25,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa