Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imeweka mikakati ya kuinua Taaluma 2023 ili kuwezesha ufaulu wa Wanafunzi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Saada Chwaya ofisini kwake kuwa mikakati ya mwaka 2023 iliyopangwa kufanya kazi ili iweze kuinua kiwango cha Taaluma pamoja na kufanya mitihani ya mwezi,mihula na ujirani mwema.
Amesema kufanya ufuatiliaji wa Shule zote mara kwa mara kwa kuongeza walimu ili kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza,kufanya vikao na walimu,Walimu wa kuu pamoja na Maafisa Elimu Kata.
“ Kuwahimiza walimu kuwa na moyo wa kujituma kufundisha inapobidi muda wa ziada ili kumaliza silabasi za masomo na kuwapa mazoezi mbalimbali”.
Hata hivyo amesema mikakati hiyo ni pamoja na kufanya ufundishaji wa makundi ili kuongeza umahiri wa Walimu,pamoja na kushirikiana na wadau wa Elimu Shule na Taasisi mbalimbali kutoa Semina za kimasomo itasaidia kuongeza uelewa wa Walimu.
Amesema mpango huo ni pamoja na kuthibiti utoro wa rejareja kwa Walimu na Wanafunzi,Kushirikiana na wathibiti ubora wa Shule ili kuweza kupata maarifa ya utunzi bora wa maswali kwa kufuata fomati mpya ya utunzi wa mitihani.
“Itasaidia kuboresha mahusiano kati ya Wakuu wa shule,walimu na walimu wa Taalumaili kuleta tija katika ufaulu”.
Pia mkakati wa kutoa elimu ya kutosha kwa uongozi wa Shule,Kamati za Shule na jamii juu ya walaka namba 3 ili kuwezesha wadau wa Elimu kuchangia maendeleo ya shule.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka:Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba.
Januari 18,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa