HALMASHAURI ya Madaba imetoa Zaidi ya Milioni 70 kwa vikundi vya wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kupitia asilimia 10.
Akitoa taarifa hiyo kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Joseph Mrimi amesema wametoa fedha kwa vikundi 24 vya wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kiasi cha Zaidi ya shilingi milioni 87 na mkopo huo umewezesha vikundi kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Mrimi amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri kwa robo ya tatu ya mwaka imetoa mikopo yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 41 kwa vikundi 11 na katika robo hii ya tatu halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 70.
Amesema vikundi hivyo vinajishughulisha na miradi ya Ujasiriamali kama usindikaji wa vyakula ,utengenezaji wa batiki,ufugaji wa mende, nyuki na mengine mengi na kupitia mkopo huo vikundi vimenunua mashine ya kukoboa mahindi.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amesema vikundi hivyo vimepewa mkopo ili waweze kujiendesha kiuchumi na kujiendesha kibiashara.
“Serikali imeweka asilimia 10 lazima itengwe na kugawiwa kwa asilimia 4 wanawake,asilimia 4 vijana na asilimia 2 watu wenye ulemavu kila mwaka na kila bajeti”.amesisitiza
Mgema amesema kwa mwaka unaoendelea bajeti ya mapato ya ndani ni bilioni moja na milioni ishirini na tatu asilimia 10 ya mapato ya ndani na katika kipindi cha miaka mitano tuweze kufikia kwenye bajeti ya milioni 500 ambazo watakopeshwa wajasiriamali.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Februari 26,2022
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa