HALMASHAURI ya Madaba imekuwa ya pili Kitaifa kwa afua za Lishe ikiwa ni sekta muhimu katika jamii.
Hayo ameyasema Mkugugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed katika kikao kazi cha maandalizi ya mipango na bajeti za afua za Lishe mwaka 2023 /2024.
Mohamed ametoa rai kwa watendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia suala nzima la Lishe ili Madaba iendelee kufanya vizuri.
“Kiujumla kama hamtasimamia tutawajibishana haiwezekani nisainishane mkataba na Mkuu wa Wilaya halafu mimi niwakumbushie madokezo na isitokee tumekuwa namba mbili kitaifa halafu tunakuwa wamwisho ”.
Amesema lengo kila mmoja atekeleze majukumu yake kufuatia mwaka wa fedha uliopita 2021/2022 umepekelea kufanya vizuri na kuchukua nafasi ya pili Kitaifa.
Hata hivyo Mkurugenzi amesema vikao vinavyofanyika lazima vilete matokeo chanya ikiwemo mtu wa Elimu,Mifugo Maendeleo ya jamamii wahakikishe wanawafikia wananchi na kutoa Elimu.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Madaba John Mapunda mara baada ya kikao hicho amesema afua za lishe ni sekta mtambuka ambayo hujumuisha idara mbalimbali ikiwemo Elimu,Mipango,Mifugo na Kilimo.
Mapunda amesema Halmashauri imechukua nafasi ya pili kitaifa ikifuatiwa na jitihada mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhamasisha ushirikiano na kuboresha katika sekta ya afya.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Novemba 10,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa