HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya Kikao cha utekelezaji wa afua za Lishe robo ya nne 2023.
Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo John Mapunda amesema mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa robo ya nne 2023 ikiwemo kufanya tathimini ya hali ya Lishe kwa Wanafunzi 135 wenye umri wa miaka 5-17 wa Shule ya Msingi Matetereka siku ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16,2023.
Amesema watoto waliokuwa na uzito uliozidi asilimia 2.9 na waliokuwa na hali nzuri ya Lishe ni asilimia 91.1 pamoja na waliokuwa na Lishe duni 6.1.
Mapunda amesema pia wamefanikiwa kufanya tathimini ya hali ya Lishe kwa watu wazima wenye umri wa mika 18 na kuendelea katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Aprili 19,2023 katika Halmashauri hiyo jumla ya watu 322 walifanyiwa tathimini, hali duni ya lishe ilikuwa asilimia 5,hali nzuri ya Lishe asilimia 66 na wenye hali ya Lishe iliyokithili asilimia 29, kutoa matone ya vitamini “A” kwa Watoto walio na umri wa miezi 6-59 wapatao 6691.
Hata hivyo Afisa Lishe amesema changamoto zilizojitokeza ikiwemo kutojengewa uwezo wa masuala ya Lishe kwa waratibu wa Lishe ngazi ya vituo vya huduma ya afya ambapo kupelekea kuathiri utoaji wa huduma sahihi za Lishe.
Ukosefu wa iodine-RTK kupelekea kutopima madini joto kwenye chumvi ngazi ya Halmashauri .
Mapunda ameitaja mikakati ya kutatua changamoto hizo ikiwemo Halmashauri kutenga fedha kupitia mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuwajengea uwezo waratibu wa vituo vya kutolea huduma za afya juu ya masuala ya Lishe,pamoja na kufanya maoteo ya mahitaji ya iodine RTK na kuwasilisha Wizara ya Afya.
Amesema kuendelea kufanya maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji ilikuwezesha elimu ya Lishe kuwafikia jamii,Pamoja na kuimarisha utoaji wa Elimu kupitia wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii na watoa huduma ngazi ya kitu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai,15,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa