HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imeingiza zaidi ya shilingi milioni 191 ya mauzo ya mazao mnadani katika msimu wa mwaka 2019/2020.
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika (W) wa Halmashauri hiyo Joseph Mrimi ameyataja Mazao ya yaliyouzwa kupitia vyama vya ushirika kuwa ni Korosho na Kahawa, Ufuta na Soya.
Mrimi amevitaja vyama vya Mazao vilivyojiunga na vyama vikuu vya ushirika MBIFACU,SONAMCU,TAMCU ikiwa kimoja kimejiunga na SONAMCU na vyama vitano TAMCU vyama viwili.
“Utaratibu wa mauzo unafanyika kwa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani ambapo vyama vinakusanya mazao ya wakulima na kupeleka mnadani na mazao hayo yakiuzwa kunakuwa na makato ya kisheria”,alisema.
Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika huyo amesema kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wakulima wanapata changamoto kama upungufu wa maghala yenye sifa,ukosefu wa Elimu ya juu ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kuchelewesha malipo ya wakulima.
Mrimi ameongeza kuwa AMCOS ni vyama vya msingi vya ushirika wa mazao na SACCOS ni vyama vya ushirika vya akiba na mikopo na ametoa rai kwa wananchi kujiunga na vyama hivyo ili waweze kunufaika.
Kwa mujibu wa Mrimi, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ina jumla ya vyama vya ushirika nane, vyama vya ushirika vya mazao(AMCOS),vitano ambavyo ni Wino (AMCOS, TAMA,AMCOS,MbangamaweAMCOS,Madaba AMCOS, (Mbonane AMCOS) na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) vitatu ambavyo ni Wino SACCOS,Muungano Gumbiro SACCO na Mahanje SACCOS.
Hata hivyo amesema Kuna baadhi ya SACCOS hazifanyi vizuri kutokana na uongozi wa SACCOS kutokuwa waaminifu,na ukosefu wa elimu ya juu na maswala ya fedha kwa watendaji wa SACCOS.
Mrimi amesema wananchi wa Madaba wananufaika na SACCOS kwa kujiwekea akiba na fursa ya kupata mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendesha shughuli zao kupitia SACCOS.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri ya Madaba
Novemba 16,2020.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa