Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imeibuka ushindi wa nafasi ya pili Kimkoa Mtihani wa Darasa la Saba kwa miaka miwili mfululizo kwa asilimia 80.89.
Hayo amesema Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Saada Chwaya ofisini kwake kuwa 2021 waliibuka kwa ushindi wa nafasi ya pili kimkoa na 2022.
“Halmashauri ya Madaba tumekuwa nafasi ya pili Kimkoa kwa miaka miwili mfululizo kwa asilimia 80.89 “.
Chwaya amzitaja Shule tano bora katika Halmashauri hiyo mwaka 2022 zilizoongoza kwa kufanya vizuri ST.Getrude wastani wa 205.27,Mkwera wastani wa 189.46,Njegea wastani wa 170.61,Kifaguro wastani wa 167.73 pamoja na Ifugwa wastani wa 164.78.
Hata hivyo ameyataja mambo yaliyosababisha kupaata ushindi wa nafasi ya pili ikiwa nipamoja na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara mashuleni,kufanya mitihani ya kutosha iliyozingatia mfumo mpya wa utunzi.
Pia kuwaandaa wanafunzi kujiamini kuanza kujitegemea wao wenyewe katika mitihani,kuwepo kwa msisitizo wa kila Shule kuwa na kamati hai za uthibiti Ubora wa ndani ya Shule ambao utaratibu wa ufundishaji na ujifunzaji,utoaji wa mazoezi, ukamilishaji wa mada,utunzi wa mtihani na ufanyaji wa masahihisho ya kina wa mazoezi ya mitihani.
Chwaya ameeleza changamoto zilizojitokeza katika ngazi ya Shule kutokuwa na walimu wa kutosha kutokana na Walimu wengi kustaafu na ongezeko la wanafunzi kila mwaka.
Amesema kukosekana kwa walimu mahiri wa baadhi ya masomo,baadhi ya Shule kutoelewa vyema mkakati wa kuongeza ufaulu kwa kufuta daraja D na E,baadhi ya Walimu kutokamilisha mada zao kwa wakati hivyo kusababisha baadhi ya mada kuto fundishwa kabisa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka:Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Januari 18,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa