HALMASHAURI ya Madaba imepitisha bajeti ya shilingi bilioni 15 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akisoma taarifa hiyo Afisa mipango Janeth Nchimbi katika baraza la Madiwani amesema Halmashauri imetayarisha mpango wa maendeleo na mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023-2025/2026 kwa kuzingatia maelekezo na miongozo mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema katika Baraza hilo ametoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani kusimamia miradi inayoendelea katika Kata zao ili kuhakikisha wanapatiwa miradi mingine.
“Unapokuwa na fedha haina sababu ya kuto Kamirisha Miradi inatakiwa kusimamia ili kazi iende haraka na kukamilika”.
Mgema katika Baraza hilo ameomba kupokea taarifa ya uandikishaji wa Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza,Darasa la kwanza pamoja na darasa la awali ikiwa umebakia mwezi mmoja kwaajili ya kukamilisha zoezi hilo.
Amesema katika wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza ni kundi muhimu sana wasipopelekwa shule watajiunga na makundi mabaya ikiwa Serikali imeshajenga madarasa kwaajili ya wanafunzi hao.
Serikali imejenga Madarasa hivyo ni wajibu wa Mzazi ahakikishe anampa mtoto mahitaji muhimu ili aanze masomo ,watendaji wa kata na Maafisa Elimu wakafanye tathimini “.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Februari 25,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa