HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imefanya tathimini ya maendeleo ya Elimu na kufikia kufanya vizuri miaka mitatu mfululizo mwaka 2018-2020.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amesema Mkutano kama huu hufanyika kila mwaka na kujiwekea mikakati ya kufanikiwa zaidi katika sekta ya Elimu.
“Tunapozungumzia tathimini ya Elimu tunawagusa moja kwa moja walimu,maswala mengine tunapoona tumekwama moja kwa moja hili swala linakuwa la walimu wametukwamisha na tukifanikiwa tunasahau kusema tumefanikiwa kwa sababu ya walimu tunaomba mtuvumilie”.
Mkuu wa Wilaya amewaomba walimu kuwa huru kuzungumza changamoto zao mambo yaliyopelekea kufanya vizuri na yaliyokwamisha kutofa fanyika vizuri katika sekta ya Elimu.
Mgema ametoa rai kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo kutoa changamoto zinazozikabili shule ambazo zipo kwenye kata zao ili ziwekewe mikakati ya kuzitatua hatimaye kufanya vizuri zaidi.
“Tunatambua uwepo wa wadau wengine kama mchango wa bank yaNMB katika Halmashauri ya Madaba wametuchangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya Elimu,pia TFS nao wametuchangia kwa kiasi kikubwa sana kama mabati,saruji tunaomba muendelee kusukuma gurudumu la Elimu katika halmashauri yetu ya Mdaba’’.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassim Mpenda katika kikao hicho amesema mbinu zinazotumika katika kuhakikisha wanafunzi wanadhulia masomo yao vizuri na kufanya zizuri darasani wameweka utaratibu wa kuwatumia watendaji,waratibu wa elimu kata katika ufuatiliaji.
Hata hivyo Mpenda amesema pia wameweka mkakati wakufanya mitihani ya muhula na nusu muhula na pale tu wanapofungua shule wanafanya mitihani iliyopelekea Halmashauri hiyo kufanya vizuri.
“ Tumeimarisha utawala bora shuleni tumekuwa na vikao vya mara kwa mara na walimu wakuu bodi za shule na vikao vya wazazi na kazi hiyo ni endelevu hata kwa walimu wanaokiuka tunawasikiliza kabla ya kuwachukulia hatua, na kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira rafiki japo siyo rafiki kwa asilimia mia moja”.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Orap Pili amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi na walimu wote kwa kazi nzuri wanayofanya na kufikia kuongoza kwa miaka mitatu mfululizo na kupata heshima kubwa katika Halmashauri ya Madaba.
Aidha Makamu Mwenyekiti ameendelea kuwaomba walimu wa Halmashauri hiyo kuwa wavumilimu kutokana na changamoto zinazojitokeza katika mazingira magumu,kwa niaba ya Madiwani amewaahidi walimu kushirikiana katika maeneo ya kazi katika kata na kufuatilia maazimia yaliyowekwa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
April 12,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa