Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imeibuka ushindi wa nafasi ya pili Kimkoa Matokeo ya kidato cha Sita Mwaka 2023 kwa asilimia 100.
Hayo amesema Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Maternus Ndumbaro ofisini kwake kuwa Madaba imekuwa nafasi ya pili Kikmkoa.
“Halmashauri ya Madaba tumekuwa nafasi ya pili Kimkoa katika Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma na kupata asilimia 100 ya ufaulu“.
Hata hivyo Afisa Elimu amesema Halmashauri ya Madaba inashule mbili zenye kidato cha kwanza hadi kitado cha Sita ikiwa Wilma wanafunzi 33 walifanya Mtihani mwaka 2023 na wanafunzi 15 wamepata daraja la kwanza na wanafunzi 17 wamepata daraja la pili mwanafunzi 1 amepata daraja la tatu.
Ndumbaro amesema Katika Shule ya Sekondari Madaba day wanafunzi 139 walifanya mtihani wa kidato cha sita wanafunzi 21 wamepata daraja la kwanza,wanafunzi 96 wamepata daraja la pili ,wanafunzi 21 wamepata daraja la tatu na mwanafunzi 1 amepata daraja la nne.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 18,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa