Kampuni mbili zinatarajia kuanza uchimbaji wa Makaa ya Mawe katika Halmashauri ya Madaba katika Kata ya Mtiyangimbole na Gumnbiro ifikapo Machi 2023.
Hayo ameyasema Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed katika kikao cha Baraza la Madiwadi cha robo ya pili ya mwaka 2022/2023.
“Tumeshapata kampuni mbili tayari zimeonyesha nia na zimetamburishwa kwa Katibu Tawala wa Mkoa na Wilaya ambazo zinatarajia kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe Machi katika Kata ya Mtiyangi Mbole”.
Hata hivyo Mkurugenzi amewaomba Waheshimiwa Madiwani wanaotoka katika Kata ya Mtiyangimbole na Ngumbiro kuwapa ushirikiano wataalamu wa uchimbaji wa makaa ya mawe.
Amesema katika uchimbaji wa Makaa ya Mawe kuna faida nyingi zitapatikana katika Halmashauri ya Madaba kwa kuongeza uwigo wa mapato ikiwa ni adhima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Wapo tayari kuhakikisha sehemu ambazo watapita na Makaa ya Mawe barabara watatengeneza wenyewe”.
Mkurugenzi amesema wananchi wa maeneo hayo ni fursa kwa kujenga Hotel pamoja na huduma zingine ikiwa ni pamoja na Halmashauri kujipatia fedha na kukua kiuchumi
“Hizo ni kampuni mbili lakini zipo nyingi ambazo zitaendelea kujitokeza kuwekeza katika Halmashauri ya Madaba hizo ni fursa kwetu kuhakikisha tunatangaza rasilimali zilizopo katika Halmashauri ya Madaba ambapo tulikuwa tunategemea kilimo pekee”.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amempongeza Mkurungenzi na wataalam kwa kufanya uchunguzi wa uchimbaji wa Makaa ya Mawe katika Kata ya Mtiyangimbole na Gumbiro amesema uchimbaji huo utasaidia kuongeza uchumi katika Halmashauri ikiwa mwanzo walitegemea mapato kupitia kilimo cha chakula.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa katika Baraza hilo amewapongeza wataalamu wote kwa utendaji kazi na hasa katika usimamiaji wa miradi ya maendeleo katika Kata zote.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Januari 23,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa