• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

HALMASHAURI ya Madaba inaardhi nzuri kwaajili ya uwekezaji wa kilimo cha mazao ya Biashara na chakula

Posted on: November 24th, 2020

HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba inamaeneo mazuri ya Uwekezaji wa Viwanda pamoja na Uwekezaji wa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na Biashara.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassim Mpenda amesema anawakaribisha wawekezaji katika Halmashauri ya Mdaba kwakuwa Ardhi ya Madaba inafaa kwa kilimo cha mazao ya Biashara,chakula na Viwanda.

‘’ kufikia Juni 2019 Halmashauri hiyo ilikuwa na wawekezaji wakubwa wa 4, Silverland Ndolela anafanya shughuli  za kilimo cha mazao na ufugaji eneo la Hekta 5,000,Wakala wa misitu Tanzania (TFS)anafanya shughuli za upandaji wa miti eneo la vijiji vya ifinga Wino na Mkongotema zaidi ya Hekta 24,000,Chuo kikuu cha Sokoine Hekta 10,000 kijiji cha Ifinga wamepanda miti zaidi 2,000,Mbangamawe partiners anazalisha chokaa katika kijiji cha Mtyangimbole”.

Aidha amesema Mwekezaji wa kampuni ya Ifinga food processing anaongeza thamani ya mazao kwa kufungasha kama Tangawizi,na Mwekezaji mwingine Kampuni ya Interfruit Limited ya Mjini Songea inatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha matunda ya Parachichi Hekari 3,000 na kujenga Kiwanda cha kusindika matunda mara yatakapoanza kuvunwa katika kijiji cha Mahanje.

Vile vile Mkurugenzi amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mdaba inazalisha mazao ya kilimo kama Miti ya Mbao,fito,nguzo za umeme/simu,kilimo cha Kahawa,Tangawizi,Matunda,Mpunga na Mazao ya Mafuta.

“Matarajio ya Halmashauri ni kupokea wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya kilimo na umwagiliaji ili watumie maeneo mazuri yaliyopo kwenye eneo letu,Kuwapokea wawekezaji wa kujenga viwanda vya kuchakata  mazao ya misitu(Miti) na Nafaka Mahindi)”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo akielezea maeneo yanayotambulika kwa kuwekeza  amesema Kitongoji cha Ifungwa kijiji cha Madaba kilo mita 10 kutoka Barabara kuu Songea- Njombe  kina Hekari 400 eneo hilo limetengwa kwaajili ya Uwekezaji wa Kiwanda  au shughuli yoyote kwa kuwekeza katika eneo hilo.

Amesema eneo la Itombolo lina Hekta 2000 lipo katika Kijiji cha Mkongotema mpakani na kijiji Lutukila kandokando ya Barabara kuu ya Songea-Njombe ni eneo lililotengwa kwaajili ya shughuri ya Viwanda vya kuchakata  mazao ya Mahindi,Tangawi na Mzao Mengine, eneo hilo ni mali ya Kijiji Halmashauri na Kijiji watahakikisha  Mwekezaji anapata Eneo analihitaji ili wananchi wanufaike na fursa na kazi zitakazoendelea eneo hilo.

Akiendelea kuelezea maeneo ya kuwekeza katika Halmashauri hiyo amesema kuna Hekta 4,200(Hekari) ni shamba la Mifugo  na ni Mali ya Wizara ya Mifugo  lipo kando ya Barabara kuu Songea-Njombe,Halmashauri ya Madaba inatunza na kulitumia amesema Wawekezaji wanakaribishwa kwaajili ya shughuri ya ufugaji  mifugo ya (Ng’ombe),kwa sasa kuna wafugaji waliokodishwa vitalu 16 na bado kuna nafasi  ya vitalu 8 na eneo limepitiwa na mto mkubwa unaowezesha kutumika kwa uzalishaji wa chakula cha Mifugo.

“Halmashauri ya Wilaya ya Mdaba inamiliki eneo lenye Hekari 500 lipo km 18 kutoka Barabara Kuu Songea Njombe ukielekea Kijiji cha Ifinga na eneo Hilo lipo tayari kwaajili ya  mwekezaji kuwekeza kwa shughuli za kilimo hasa kilimo cha Miti,Kahawa,na Mazao mengine yanayoendana pamoja na maporomoko ya Umeme Masigira,Lipupuma,na Lingatunda”.

Pia Halmashauri ya Madaba na vijiji vyake 21 inamaeneo ya kutosha hivyo yeyote anakaribishwa kuwekeza katika maeneo hayo na vijiji 11 vimepimwa Halamashauri itahakikisha mwekezaji anapata eneo la kutosha analohitaji katika kijiji chochote kwa kilimo cha mazao.

Halmashauri ya Madaba inatoa rai kwa wawekezaji kuwekeza katika Viwanda mbalimbali kwenye mji wa Madaba na Vijijini ikiwa tayari vijiji 19 vinaumeme wa uhakika,kutokana na malighafi zilizopo Viwanda vya uchakataji wa Mazao ya Misitu  na Usindikaji.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Halmashauri ya Madaba

Novemba 24,2020.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa