HALMASHAURI ya Madaba imepitisha bajeti kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 14 kwa kuzingatia vipaumbele vinne.
Akisoma taarifa hiyo afisa mipango Prosper Luambano katika kikao cha Baraza la Madiwani cha makadirio ya mpango na bajeti kwa mwaka 2023/2024.
Amesema bajeti hiyo imezingatia maeneo ya vipaumbele vya Halmashauri katika mpango na bajeti ya Wilaya ya Madaba kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Hata hivyo amesema Halmashauri kupitia viongozi mbalimbali waliofanya ziara kutembelea Halmashauri hiyo wamezingatia vipaumbele vya maeneo manne ikiwemo kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kubuni nyanzo vipya na kuimarisha vyanzo vilivyopo.
Kuimarisha upatikanaji na utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na Halmashauri kutenga fedha kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa kituo cha afya,zahanati,miundombinu ya madarasa,ununuzi wa dawa na vitendanishi na vifaa tiba.
Luambano amesema kipaumbele kingine kitakachozingatiwa ni pamoja na kuboresha utawala bora na utawala wa kisheria pamoja na Halmashauri kuwa na utaratibu wa kufanya maamuzi na kutekeleza kwaajili ya maendeleo na ustawi wa jamii unaozingatia msingi na utu,haki,ushirikishwaji,demokrasia,uwajibikaji,uwazi,utekelezaji,tija,ufanisi,usawa wa makundi yote.
“Kuimarisha ufuatiliaji,usimamizi na tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa na Halmashauri,wananchi na wadau mbalimbali”.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Olaph Pili kwa niaba ya Mwenyekiti Teofanes Mlelwa akifunga kikao hicho cha bajeti cha Baraza la Madaiwani mara baada ya Madiwani kuunga mkono bajeti hiyo ametoa rai kwa Madiwani kushirikiana na wataalam wa Halmashauri hiyo kusimamia miradi iliyoelekezwa katika ngazi ya Halmashauri hadi Kata ikiwemo ya Elimu na Afya.
“Pia Halmashauri yetu ni ya Kilimo tuhakikishe tunaondoa migogoro ya wafugaji na wakulima mwaka huu tuhakikishe tunaimaliza ili mwakani mambo yawe safi.
Hata hivyo amewapongeza wataalamu kwa kuandaa bajeti hiyo kwa kuonyesha stahiki za madiwani,pamoja na kuweka kipaumbele katika makusanyo pamoja na kuweka vipaumbele katika sekta ya Elimu na Afya.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Februari 4,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa