Mjumbe wa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Hawa Ghasia amefanya ziara yake Katika Jimbo la Madaba na kutembelea ujenzi wa Madarasa unaojengwa kupitia Mradi wa BOOST katika Shule ya Msingi Ngembambili.
Mradi huo wa Madarasa mawili na matundu 3 ya vyoo unaojengwa kwa shilingi Milioni 53,100,000/= na kufikia hatua ya ukamilishaji.
Ghasia akimwakilisha Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda amesema mradi umefikia hatua nzuri ikiwa na makosa madomadogo ya kurekebisha ili mradi uweze kukamilika na wanafunzi waweze kutumia madarasa hayo.
Hata hivyo amewasisitiza wazazi kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria masomo ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Miundombinu ya Shule na kuhakikisha wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia.
“Hayo Madarasa tuliyojengewa tumepewa na Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan anahakikisha nyie wanafunzi wa Ngembambili mnapata Madarasa kwahiyo mjitaidi kusoma ili baadae mjekuwa madaktari,wabunge na viongozi wengine”amesema Ghasia.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 26,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa