DIWANI Mpya Kata ya Mtyangimbole Twaib Ngonyani ameapishwa rasmi tangu kuchaguliwa kwake Septemba 19,2023 na kupata kura asilimia 97.
Mara baada ya kuapishwa Ngonyani amesema atahakikisha anasimamia miradi ambayo imeanzishwa na aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo wakati wa uhai wake Erick Mkorwe.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa Maji wa Bilioni 5,ujenzi wa Barabara kutoka Mtiyangimbole hadi kakong’o na ukarabati wa madarasa manne katika Shule ya Msingi Ruhimba ambapo Milioni 90 imeletwa na Serikali.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Novemba 11,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa