MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amewaasa walimu kuacha kukopa mikopo kausha damu ili kuepuka msongo wa mawazo.
Hayo amesema katika kikao kilichojumuisha walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari walipozungumza na afisa elimu Mkoa wa Dodoma Vicent Kayombo aliyemwakilisha Katibu Mkuu ofisi ya Rais TAMISEMI Adolf Ndunguru.
Mohamed amesema kupitia mikopo kausha damu inapelekea walimu kutofundisha kwa weledi na matokeo yake kupelekea kufeli kwa wanafunzi.
“Walimu hakikisheni mnajilinda na afya zenu achani kulewa hovyo sote tumepita mikononi mwa walimu nyie ni watu muhimu sana”.
Aidha Mkurugenzi ameomba serikali usimazi wa miradi ya maendeleo ijengwe kupitia mkandalasi badala ya kutumia force account ili walimu wapate mda mwingi wa kufundisha.
“Mirdi ya maendeleo inaleta shida mwalimu akiletewa mradi anadai kuacha ukuu wa shule naomba mtufikishie kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miradi ya elimu itumie mkandarasi ili walimu wapate mda mwingi wa kufundisha”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Juni 1,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa