Timu ya Menejimenti halmashauri ya Wilaya wa Madaba imepewa mafunzo ya kanuni ya usimamizi wa mikopo ya asilimia 10.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akifungua mafunzo hayo ametoa rai kwa menejimenti hiyo ya usimamizi wa mikopo kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake katika majukumu yake ya kazi.
“Naamini baada ya mafunzo haya kila mmoja atakuwa ameiva kwaajili ya utekeleza wa majukumu ambayo tumepewa”.
Naye Afisa maendeleo ya Jamii wa halmashauri ya Wilaya ya Madaba Juma Komba akitoa mafunzo kwa menejimenti hiyo ameyataja malengo mahususi ya mafunzo hayo ikiwa ni kuongeza uelewa wa kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wananwake,vijana na watu wenye ulemavu.
“Kufafanua taratibu za utambuzi,utoaji,usimamizi,ufuatiliaji na urejeshaji wa mikopo ya vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu”.
Aidha amesema mafunzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano na uratibu wa usimamizi wa mikopo baina ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI,Ofisi za Wakuu wa Mikoa,mamlaka za Serikali za Mitaa,taasisi za Serikali,taasisi za fedha,asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Oktoba 28,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa