MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed anawataarifu Umma kuwa kuanzia leo tarehe 13 hadi 14 Septemba unafanyika Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi Kitaifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Madaba inajumla ya watahiniwa 1464 ikiwa wavulana 712 na wasichana 752 ikijumuisha Shule 29 ambapo wanafunzi wanaungana na wenzao kote nchini kufanya Mtihani huo wa Kumaliza Elimu ya Msingi kwa Mwaka wa Fedha huu 2023.
Mkurugenzi anawatakia kila la kheri watahiniwa wote wa Darasa la 2023 katika mitihani yao ya kumaliza Elimu ya Msingi na kuwaombea wafanye vyema na kuzingatia taratibu za Mitihani.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Septemba 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa