• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

DED Madaba awapongeza wananchi wa Kata ya Gumbiro Kuunga Mkono Jitihada za Rais Samia

Posted on: October 20th, 2023

MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amewapongeza wananchi wa Kata ya Gumbiro kwa kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa usimamizi wa utekelezaji wa  Miradi iliyoletwa katika Kata hiyo.

Hayo amesema alipozungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha Ngadinda na kubainisha miradi iliyotekelezwa ikiwemo Madarasa  mawili na matundu 3 ya vyoo  kupitia mradi wa Boost jumla ya shilingi Milioni 53,100,000/=zimetumika, Shule ya Msingi Sokoine zaidi ya shilingi Milioni 34 zimetumika kwaajili ya ujenzi wa matundu 13 ya vyoo kupitia mradi wa SWASH.

“Mwaka 2023/2024 katika Kata hiyo wanatarajia kupokea zaidi ya shilingi Milioni 106 na kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo”.

Hata hivyo Mkurugenzi ametoa rai kwa wazazi kuwalinda watoto na kuwahimiza kusoma ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa fedha kwaajili ya kuboresha Miundombinu ya Shule.

Diwani Kata ya Gumbiro Gustaph Tindwa ameipongeza Serikali kwa kuleta fedha kwaajili ya  utekelezaji wa  miradi ya maendeleo katika kata hiyo  amesema mradi wa barabara  utakaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 200 unaotekelezwa na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA).

“Hizo zote ni pongezi za Rais Samia,Mbunge wa Jimbo la Madaba na  wewe Mkurugenzi wa Halmashauri   ikiwa wananchi wa Kata ya Gumbiro  wananufaika na miradi hiyo”.

Tindwa amesema pia mradi wa Maji unatekelezwa katika Kata hiyo kwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja utakaowasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya  maji.

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba

Oktoba 20,2023.

 

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa