HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya Hafla fupi ya pongezi kwa Shule na walimu waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne mwaka 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo akizungumza katika Hafla hiyo amewapongeza walimu hao na ametoa rai kuhakikisha Halmashauri inaendelea kushika nafasi ya kwanza Kimkoa.
“Kwa mwaka 2023/2024 Halmashauri yetu ya Madaba imeendelea kufanya vizuri sana katika ufaulu kwa upande wa Sekondari na Elimu Msingi”.
Hata hivyo Mkurugenzi amesema jitiahada za ufaulu katika Halmashauri imepelekea kuwa na miundombinu mizuri ya Elimu na kuwapa motisha walimu na kuwapandisha madaraja.
“Mhe.Rais anafanya kazi kubwa sana katika swala la Elimu ameboresha miundombinu ya Elimu na kuwapa motisha walimu tuchukue hatua hii kumshukuru sana”.
Aidha Mkurugenzi ametoa rai kwa walimu hao kupitia motisha aliyotoa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha wanafundisha kwa bidii na kuhakikisha wanafunzi wanafauru.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Julai 10,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa