HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wamefanya Kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili kuanzia Oktoba hadi Disemba 2023.
Akizungumza katika Baraza hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed ametoa taarifa ya wanafunzi walioripoti Shuleni Januari 2024.
Amesema wanafunzi wa awali walioripoti shuleni na kuanza masomo ni 1691 sawa na asilimia 101.9, wanafunzi wa darasa la kwanza maoteo yalikuwa 1695 na hadi kufikia sasa wameripoti wanafunzi 1684 sawa na asilimia 99
Hata hivyo amesema Elimu Sekondari walipangiwa wanafunzi 1254 kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2024 hadi kufikia sasa wameripoti wanafunzi 934 sawa na asilimia 74.46.
Mkurugenzi ametoa rai kwa Madiwani na Watendaji Kata kuendelea kuwahamasisha wananchi kupeleka watoto shuleni kwa wakati.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Januari 31,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa