MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amefanya kikao kazi na waganga wafawidhi wa hospitali,vituo vya afya na zahanati.
Katika kikao hicho kimelenga uhamasishaji wa matumizi ya mfumo wa GOTHOMIS katika vituo vya kutolea huduma ya afya na kuongeza ukusanyaji wa mapato katika halmashauri.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ametoa maelekezo ikiwemo msimamizi wa kituo anatakiwa kuhakikisha dawa zote zinaingia katika mfumo wa GOTHOMIS mara zinapofika kituoni,kuingiza vipimo vya maabara katika mfumo,kuhakikisha nyaraka zinaonyesha kuna uhalali wa msamaha kwa wagonjwa na kuhakikisha huduma zote zinatolewa kwenye mfumo.
Aidha Mohamed amesema ofisi ya mganaga mkuu (CHMT) kuhakikisha vituo vya kutolea huduma vinakuwa na miundombinu kwaajili ya mfumo wa GOTHOMIS,vituo vyote vinakuwa na mfumo wa GOTHOMIS,Vituo vyote vihakikishe vinatoa taarifa ya fedha kwa kutumia mfumo wa GOTHOMIS na kutoa taarifa kila siku juu ya mwenendo wa utumiaji wa mfumo.
“Watendaji kata wawajibike kwa kuwa mfumo ni mkakati wa uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato hivyo watendaji wa kata watawajibika kufuatilia utendaji kazi katika maeneo yao”.
Amesema kila kituo cha kutolea huduma ikiwa ni pamoja na elimu msingi na sekondari na afya wanatakiwa kuhakikisha wanatumia mifumo yote kwa usahihi kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa ukiwemo mfumo wa NEST,GOTHOMIS na FFARS.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 27,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa