MKURUGENZI Mtendaji Sajidu Idrisa Mohamed leo Oktoba 11,2023 amekagua mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji,wodi ya wanawake na wanaume unaoendelea kujengwa kwa shilingi milioni 800 katika Hospitali ya Wilaya ya Madaba.
Hospitali hiyo inayojengwa kwa awamu ameweza kukagua Wodi ya Watoto pamoja na kujinea vifaa vya Hospitali ambavyo kwa asilimia kubwa vimenunuliwa.
Hata hivyo Mkurugenzi amezungumza na watumishi na kusikiliza changamoto zinazojitokeza katika Hospitali hiyo ikiwemo baadhi ya Majengo kutokamilika ikiwa huduma zinaendelea kutolewa kwa wananchi.
Fanti Abbasy ambaye ni kaimu mratibu wa huduma za Maabara amesema changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika Hospitali hiyo jengo la maabara kuto kuwa na milango,ukosefu wa vitanda vya kutolea huduma kwa wagonjwa pamoja na maji ya uhakika ikiwa huduma za afya zinaendelea kutolewa.
Abbasy amesema pia Mkurugenzi ameangalia vifaa vya Hospitali hiyo ambavyo vipo katika Maabara ikiwemo Darubini inayotumika katika uchunguzi wa Magonjwa.
“ ametoa maagizo kwa mamlaka zinazohusika kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa Maji zinakamilika kwa wakati ”.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 11,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa