MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amefanikiwa kutatua mgogoro wa Mipaka ya Vijiji Kata ya Ngumbiro.
Hayo ameyasema Diwani wa Kata hiyo Gustaph Tindwa katika Mkutano wa wananchi ambapo Mkurugenzi amesikiliza kero pamoja na changamoto zinazo wakabili wananchi hao.
Tindwa amewapongeza Viongozi wa Halmashauri ya Madaba kwa kumaliza kero ya Mipaka ya Vijiji vya Mbangamawe,Ngadinda na Gumbiro kwa kuweka mipaka sawa ikiwa mgogoro huo umeanza Mwaka 2002 na kumalizika Mwaka 2023.
“Niwapongeze wataalam kwa ushirikiano mzuri na Mkurugenzi tumemaliza migogoro iliyoanza mwaka 2002 mwaka huu 2023 tumeweka mambo sawa ”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 20,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa