MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amesikiliza kero na malalamiko ya watumishi na kuzitatua.
Mohamed akisikiliza kero hizo ametoa rai kwa watumishi kuwa ni kikao cha kawaida ambacho wawehuru kuzisema changamoto zao na mazuri ambayo wanayapata katika eneo la kazi na kushauriana ili waweze kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano.
“Watumishi wote mpo hapa katika kada zote Elimu ,Afya,na watendaji wengine naomba niwasikilize wala msisite kusema chochote hata ushauri itasaidia kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na kanuni”.
Hata hivyo amewataka wakuu wa idara kufanya vikao na wasaidizi wao na kusikiliza kero zao kila mwezi ili kupunguza malalamiko ya watumishi.
Mkurugenzi amewapongeza watumishi hao kwa kuendelea kumpa ushirikiano katika utendaji kazi na usimamiaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo na kupelekea Rais Samia kuendele kumwamini.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilayaya Madaba
Machi 26,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa