MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed ameongoza kikao cha wadau wa Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri hiyo Juni 15, 2024 na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Akizungumza katika kikao hicho amewaagiza watendaji wa Kata,Vijiji,Maendeleo ya jamii Kata na Maafisa elimu Kata kufanya uhamasihaji kwa wananchi juu ya ujio wa Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri hiyo.
Aidha amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo kuhakikisha eneo la mkesha wa Mwenge wa Uhuru huduma zote za Afya zinakuwepo na kutolewa kwa wananchi.
“Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2024 tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Mei 30,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa