MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri Halmashauri ya ya Wilaya ya Madaba amemshukuru Rais Samia kwa kumwamini na kuendelea kumpa nafasi ya Ukurugenzi katika Halmashauri hiyo.
Hayo amesema alipofungua Mafunzo ya Mfumo wa FFARS kwa Watendaji Kata,Vijiji na walimu wa Sekondari na Msingi yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Hata hivyo Mkurugenzi amewashukuru na kuwapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo kwa ushirikiano katika kazi kuanzia alipoteuliwa na Rais takribani mwaka mmoja na miezi 10.
“Leo tarehe 7 tunaanza majukumu mengine nawategemeeni sana tuendelee kufanya kazi kwa pamoja na ninyi watumishi wenzangu”.
Hata hivyo Mkurugenzi amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kumwamini na kumpa nafasi kwa mara nyingine ya kuongoza Halmashauri ya Madaba.
Mohamed amesema kuanzia sasa watumishi na Mkurugenzi watakuwa na mbinu mpya ya kuhakikisha kazi na majukumu ya Halamshauri yanaenda kwa pamoja na kwa mafanikio makubwa.
Mkurugenzi amewaagiza watendaji na walimu kusimamia miradi ya Boost ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora kwasababu ni miradi ya Lipa kwa matokeo.
“Mkitoka hapa mkaongeze mafundi na mfanye kazi usiku na mchana ili tusivuke na miradi hiyo kwa mwaka wa fedha mpya 2023/2024”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halamshauri ya Madaba
Juni 7,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa