Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amemuunga Mkono Rais Samia kwa kutoa zawadi za sikukuu ya Chrismas na Mwaka mpya 2025 katika kituo cha watoto yatima Malaika childrens home Mahanje.
Afisa ustawi wa Jamii Shani Kambuga amemwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo katika kuwasilisha zawadi hizo zilizoghalimu shilingi laki nane na nusu (850,000/=) zikiwemo Soda,Mchele kilo 100, Mbuzi mmoja,sabuni na mafuta ya kupaka.
“Zawadi hizi zimetolewa na ofisi ya Mkurugenzi kwa kumsapoti Mhe.Rais Samia kwaajili ya watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kufurahia sikukuu ya Chrismas na Mwaka Mpya katika kituo hiki cha Mahanje ”.
Msimamizi wa kituo hicho cha Malaika childrens home Mahanje Sister Melina Haule amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwa kumsapoti Rais Samia kwa kutoa zawadi ya sikukuu kwa watoto yatima Mahanje.
“Namshukuru Mkurugenzi kwa kutoa msaada katika kituo chetu tumefurahi na tumepokea kwa furaha na utatusogeza mbele na tuna watoto 26 “.
Moja kati ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho Ana Mgina amemshukuru mkurugenzi kwa kutoa sapoti yake kwa kutoa zawadi za sikukuu ambazo zitawasaidi kula vizuri mwaka mpya.
“Tunashukuru sana kwa zawadi zenu mlizotuletea tunaomba Mkurugenzi utufikishie salamu kwa Mama Samia mwambie asante watoto tumefurahi Mungu awabariki”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 1,2025.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa